Overblog
Edit post Follow this blog Administration + Create my blog

Ushauri wa Arsene Wenger kwa Thierry Henry kama anataka kupata mafanikio katika ukocha…

by Japhet Restus

posted in sport

Ushauri wa Arsene Wenger kwa Thierry Henry kama anataka kupata mafanikio katika ukocha…

Kocha wa klabu ya Arsenal ya Uingereza Arsene Wenger ambaye amewahi kumfundisha Thierry Henry kama mchezaji wake kwa miaka mingi, Wenger amemshauriThierry Henry kama kweli ana nia ya dhati ya kutaka kupata mafanikio kama kocha katika soka.

Wenger amemshauri Henry ambaye kwa sasa anaifundisha timu ya Arsenal chini ya umri wa miaka 18 kuwa, kama kweli anataka kupata mafanikio katika ukocha inabidi apate ushauri wa kisaikolojia katika akili yake. Henry anafundisha kikosi hicho cha vijana huku akipata mafunzo ya ukocha.

Henry ambaye anaheshima ya kuwa mfungaji bora wa klabu ya Arsenal kwa muda wote, alisajiliwa na Wenger akitokea klabu ya Juventus ya Italia mwaka 1999 ila Wengeramemueleza utofauti uliyopo kati ya kuwa mchezaji na kuwa kocha.

To be informed of the latest articles, subscribe:
Comment on this post